
Friday, April 5, 2013
TUNAWEZA KUCHEZA BILA MESSI - ALVES.
BEKI wa klabu ya Barcelona, Dani Alves amesema kikosi cha timu hiyo kinaweza kucheza bila kuwepo kwa mshambuliaji wake nyota Lionel Messi katika mchezo dhidi ya Real Mallorca kesho. Messi ambaye ambaye ni anashikilia tuzo nne za mwanasoka bora duniani aliumia msuli wa paja katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint Germain maumivu ambayo yatamuweka nje katika mchezo huo wa kesho . Alves amesema timu hiyo inaweza kucheza kwa kiwango chake cha juu hata kama watamkosa nyota huyo kwenye mchezo huo na kuonyesha kwamba wanaweza kufanya vizuri hata bila uwepo wake. Mbali na kukosekana kwa Messi, Barcelona pia watakosa huduma ya mabeki wake tegemeo Javier Mascherano na Carles Puyol ambao wanajiuguza. Katika mchezo huo kocha wa timu hiyo Tito Vilanova atarejea kwa mara ya kwanza katika benchi la ufundi kwenye uwanja wa Camp Nou toka alipokwenda kwenye matibabu ya kansa jijini New York, Marekani Januari mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment