Friday, April 5, 2013

MCHEZO WA DC MOTEMA PEMBE NA TP MAZEMBE WASIMAMISHWA KWA AJILI YA MAOMBOLEZO.

SHIRIKISHO la Soka la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC limesimamisha mchezo wa Ligi Kuu kati ya timu ya DC Motema Pembe na TP Mazembe ambao ulikuwa uchezwe April 14 mwaka huu kufuatia vifo vya wachezaji wa Motema Pembe wiki iliyopita. Hakuna tarehe nyingine iliyopangwa kwa ajili ya mchezo huo huku uongozi wa Motema Pembe pia ukitangaza kuwa hawatasafiri kwenda jijini Bujumbura, Burundi kucheza na timu ya Lydia LB Academy ambao ni mchezo wa Kombe la Shirikisho. Golikipa wa kimataifa Guelaor Dibulana, mshambuliaji Hugues Muyenge na kiungo Mozart Mwanza walikufa katika ajali ya gari wakati wakitokea katika kanisa la Saint-Dominique jijini Kinshasa Alhamisi iliyopita. Rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter Jumanne alituma salamu za rambirambi kwa familia za wachezaji hao, shirikisho na wadau wote wa soka katika nchi hiyo kwa pigo kubwa walilopata.

No comments:

Post a Comment