MENEJA wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho, yuko tayari kumfanya Xabi Alonso kuwa usajili wake wa kwanza Stamford Bridge katika kipindi cha majira ya kiangazi kama akirejea kuifundisha klabu ya Chelsea. Mourinho alibainisha Jumanne usiku mara baada ya Madrid kung’olewa katika Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka Santiago Bernabeu katika kipindi cha majira ya kiangazi. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 amesema atakwenda kule anapodhani anapendwa kauli ambayo watu walichukulia kwamba atarejea Chelsea ambako ameiongoza klabu hiyo kushinda mataji matatu kabla ya kuondoka mwaka 2007. Inaeleweka kuwa Mourinho tayari amemtaja nyota wa zamani wa Liverpool Alonso kama mmoja wa wachezaji atakaondoka nao kama akirejea Chelsea kuchukua nafasi ya Rafa Banitez. Alonso mwenye umri wa miaka 31 ambaye alishinda taji la LIgi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Liverpool mwaka 2005 mkataba wake unaishia mwakani na bado hajasaini mkataba mwingine wa miaka miwili aliopewa na Madrid.
No comments:
Post a Comment