
Saturday, May 4, 2013
PLATINI ATAKA MAZUNGUMZO YA WAAMUZI KUREKODIWA.
RAIS wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Michel Platini amebainisha nia yake ya kutaka kurekodi mazungumzo kati ya waamuzi katika mechi za soka za Ulaya mapema msimu ujao. Platini amesema amekubali makosa ya mwamuzi ambaye hakuona mchezo mbaya aliocheza Thomas Mueller dhidi ya Jordi Alba na kupelekea Barcelona kufungwa bao la tatu na Bayern Munich katika ushindi wa mabao 4-0 waliopata katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini Platini ameendelea kusema kwamba huwa kunakuwa na waamuzi watatu wa kimataifa na hakuna hata mmoja aliyeliona tukio hilo hapo lazima kutakuwa na tatizo. Platini amesema kama mwamuzi wa kati angekuwa peke yake asingeweza kuona tukio hilo na hata wa pili lakini ukisema wote watatu hawakuliona tukio hilo ni suala lisilowezekana kabisa ndio maana meamua kuanzia msimu ujao mazungumzo yao yote yawe yanarekodiwa ili kujua tatizo lilipo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment