
Saturday, May 4, 2013
TAIFA STARS YAPANGWA NA NAMIBIA, MAURITIUS NA SWAZILAND KATIKA MICHUANO YA COSAFA.
TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajiwa kukutana na timu ngumu ilizopangiwa katika kundi A kwenye ratiba ya michuano ya inazozishirikisha nchi zilizopo kusini mwa Afrika-COSAFA iliyopangwa jana jijini Lusaka, Zambia. Katika kundi A Taifa Stars imepangwa kuchuana na timu za Namibia, Mauritius na Swaziland ambapo mshindi katika kundi hilo atakutana na Afrika Kusini katika mchezo war obo fainali. Stars itakwaana na Swaziland Julai jijini Lusaka kabla ya kukutana na Mauritius Julai 8 hapohapo Lusaka huku mchezo wa mwisho dhidi ya Namibia ukitarajiwa kuchezwa Julai 10 jijini Kabwe. Stars ambao kwa kipindi cha hivi karibuni wameonyesha kuwa na kiwango cha kutisha wanategemea kushinda michezo yao na kuibuka mshindi kwenye kundi hilo na kutinga hatua ya robo fainali kucheza na Bafana Bafana ambao ni mabingwa mara tatu wa michuano hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment