Saturday, July 13, 2013

AUBAMEYANG AWASHANGAZA WAAJIRI WAKE KWA KASI YAKE ZAIDI YA BOLT.

MSHAMBULIAJI mpya wa kabu ya Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang amewashangaza waajiri wake wapya baada ya kukimbia kwa kasi kuliko mwanariadha nyota wa mbio fupi Usain Bolt wa Jamaica. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alikimbia mita 30 kwa kutumia muda wa sekunde 3.7 wakati wa mazoezi ya Dortmund kujiandaa na msimu mpya jijini Bad Ragaz, Switzerland. Aubamuyang alitumia sekunde moja zaidi ya Bolt wakati akivunja rekodi ya dunia katika mashindano ya riadha ya dunia yaliyofanyika huko Berlin katika mbio za mita 100 mwaka 2009. Nyota huyo ambaye alijiunga na Dortmund kwa ada ya euro milioni 13 kutoka klabu ya Saint-Etienne wiki iliyopita alicheza mechi ya kwanza akiwa na klabu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Basel ambao walishinda kwa mabao 3-1.

No comments:

Post a Comment