Saturday, July 13, 2013

WENGER AANZA MAZUNGUMZO YA MKATABA MPYA ARSENAL.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameahidi kuendelea kuwepo klabuni hapo baada ya kubainisha kuwa tayari ameanza mazungumzo juu ya mkataba mpya. Mkataba wa kocha huyo Mfaransa unamalizika katika kipindi cha majira ya kiangazi mwakani hivyo kuzusha tetesi kuwa msimu ujao unaweza kuwa wa mwisho kwa kocha huyo. Lakini Wenger amesisitiza nia yake ya kuongeza mkataba wake wenye thamani ya paundi milioni saba kwa msimu na tayari mazungumzo ya awali na Ofisa Mkuu wa klabu hiyo Ivan Gazidis yameshaanza. Akihojiwa kuhusiana na hilo Wenger ameanza kuinoa Arsenal mwaka 1996 amesema bado angependa kuwepo Emirates na kuthibitisha kuanza kwa mazungumzo ya mkataba ya mpya.

No comments:

Post a Comment