Wednesday, July 17, 2013
DORTMUND WATAMALIZA UBABE WA BAYERN MSIMU HUU - SAHIN.
KIUNGO wa klabu ya Borussia Dortmund, Nuri Sahin ameonyesha shauku kwa usajili uliofanywa na klabu hiyo huku akiwa na matumaini ya kupiku utawala wa wapinzani wao Bayern Munich katika soka la Ujerumani. Ujio wa wachezaji kama Pierre-Emerick Aubameyang, Henrikh Mikhitaryan na Sokratis Papastathopoulous katika kikosi cha Jurgen Klopp kunategemewa kuisimamisha Bayern kurudia mafanikio ya kushinda mataji yote matatu nchini humo. Sahin, ambaye amebakisha miezi 12 ya mkopo kutoka klabu ya Real Madrid ana matumaini usajili huo unaweza kuwaongezea nguvu ili kupambana na Bayern ambao kwasasa wametawala soka la nchi hiyo. Dortmund walitolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na DFB-Pokal na Bayern msimu uliopita huku pia wakimaliza nyuma kwa alama 25 mbele ya Bayern ambayo ndio walikuwa mabingwa wa Bundesliga.
No comments:
Post a Comment