Thursday, July 18, 2013

SHABIKI WA VIETNAM ALIYEKIMBIZA BASI LA ARSENAL KWA KILIMETA TANO ADAI KUALIKWA JIJINI LONDON.

SHABIKI wa soka wa Vietnam ambaye alilikimbiza basi lililokuwa limebeba wachezaji wa Arsenal katika mitaa ya jiji la Hanoi wakati timu hiyo ikiwa nchini humo amedai kuwa amealikwa kwenda jijini London kushuhudia moja ya mechi ya timu hiyo. Shabiki huyo anayejulikana kama Vu Xuan Tien alionyeshwa katika picha za video katika mtandao wa klabu hiyo akilikimbiza basi hilo huku wachezaji wakimshangilia huku wakimtania kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger kumsajili kutokana na bidii na mazoezi aliyokuwa nayo. Baada ya kulikimbiza basi hilo kwa muda wa umbali wa kilometa tano hatimaye lilisimama na shabiki huyo kuingia ndani kupiga picha na wachezaji wa klabu hiyo huku fulani yake ikiwekwa saini na Wenger. Shabiki huyo ambaye ni kijana mwenye umri wa miaka 20 amedai kuwa ametimiza ndoto zake na hatakuja kusahau kamwe katika maisha yake huku akidai kualikwa kwenda kushuhudia moja ya mechi za klabu hiyo katika Uwanja wa Emirates katika kipindi cha Agosti na Septemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment