Wednesday, July 17, 2013

SINA WASIWASI KWASABABU MAWAKILI WANGU WATALITATUA TATIZO LA KODI - MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi ana matumaini na mawakili wake kutatua tatizo lake la kodi baada nyota huyo na baba yake kutuhumiwa kukwepa kodi na mamlaka za nchini Hispania mwezi uliopita. Messi na baba yake Jorge ambao wote walikana tuhuma hizo za kukwepa kulipa kodi ya kiasi cha euro milioni nne katika kipindi cha mwaka 2006 mpaka 2009. Akihojiwa Messi amesema hana wasiwasi katika hilo kwani ahajawahi kufanya shughuli hizo peke yake wala kwa kumshirikisha baba yake. Messi amesema wamewaachia suala hilo mawakili na mameneja wao kulishughulikia na wanaamini watalimaliza ili kuondoa utata uliojitokeza. Kwa mujibu wa gazeti la Forbes la Marekani Messi ni mmoja ya wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani akitia kibindoni kitita cha dola milioni 20 kwa msimu ikiwa ni sehemu ya mshahara wake na marupurupu mengine.

No comments:

Post a Comment