MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Gareth Bale anatarajiwa kukosa mchezo wa kirafiki kati ya timu yake na Monaco ya Ufaransa kutokana na majeruhi yanayomsumbua. Kwa mujibu wa mtandao wa The Sun mshambuliaji wa kimataifa wa Wales aliagana na wachezaji wenzake jijini London mapema Ijumaa kabla ya hawajapaa kuelekea jijini Monte Carlo kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki. Mbali na kuukosa mchezo huo Bale pia anatarajiwa kuukosa mchezo wa kirafiki wa timu yake ya taifa ya Wales dhidi ya Ireland unaotarajiw akupigwa jijini Cardiff Agosti 14 mwaka huu. Wakati Bale akipambana kurejea katika hali yake ya kawaida, mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy anatarajiwa kukaa chini kwa mara ya kwanza kuzungumza na rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez jijini Miami wiki ijayo kwa ajili ya mazungumzo juu ya uhamisho wa mchezaji huyo. Kama mazungumzo hayo yakienda vizuri, Bale mwenye umri wa miaka 24 anatarajiwa kuwa mchezaji mwenye thamani zaidi, heshima ambayo kwasasa inashikiliwa na Cristiano Ronaldo ambaye alihama kutoka Manchester United kwenda Madrid kwa ada ya paundi milioni 80 mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment