BINGWA wa zamani wa michuano ya olimpiki, Denise Lewis amedai kuwa mwanadada nyota katika mbio za kuruka chini Jessica Ennis-Hill anaweza kupoteza zaidi kama angeshiriki michuano ya riadha ya dunia ambayo inatarajiwa akufanyika baadae mwezi huu. Ennis-Hill ambaye ni bingwa wa olimpiki katika mbio za kuruka chini mapema jana aliamua kujitoa katika michuano hiyo itakayofanyika jijini Moscow kutokana na majeraha yanayomsumbua. Lewis ambaye naye aliwahi kuwa bingwa wa mbio hizo miaka 13 iliyopita katika michuano iliyofanyika jijini Sydney amesema mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Marekani alifanya uamuzi wa busara kujitoa. Ennis-Hill ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya kisigino alijitoa katika mashindano matano tofauti kuanzia Mei na Julai kabla ya kushiriki mashindano ya Diamond League ya Uingereza ikiwa ni mara ya pili kushindana toka anyakue medali ya dhahabu katika michuano ya olimpiki mwaka jana.
No comments:
Post a Comment