Friday, August 2, 2013

ITAKUWA NGUMU BALE KUICHOMOLEA MADRID - REDKNAPP.

MENEJA wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Harry Redknapp amedai kuwa itakuwa ni ngumu kwa Gareth Bale kukataa kwenda katika klabu ya Real Madrid ya Hispania. Meneja wa Madrid, Carlo Ancelotti alibainisha mapema kuwa vigogo hao wa soka nchini humo wako katika mazungumzo ya kujaribu kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 24. Redknapp amesema anadhani itakuwa ngumu kwake kutokubali kuondoka sasa kwani ameshasikia kutoka katika vyanzo tofauti kwamba anataka kuondoka katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi. Kumekuwa na taarifa kuwa Madrid wanajiandaa kutoa ofa itakayovunja rekodi ya dunia ya paundi milioni 80 waliyomsajili Cristiano Ronaldo kutoka Manchester United mwaka 2009 ingawa mpaka sasa hakuna ofa rasmi iliyotolewa. Redknapp amesema Madrid ni klabu ya kipekee ambapo mchezaji yoyote ana ndoto ya kuichezea siku moja hivyo kukataa ofa yao huwa ni ngumu kwa mchezaji yoyote.

No comments:

Post a Comment