Friday, August 2, 2013

SAA KUBWA ILIYOWEKWA KATIKA UFUKWE WA COPACABANA KUHESABU MUDA ULIOSALIA KABLA YA KUANZA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA YASHINDWA KUFANYA KAZI.

SAA kubwa ambayo inahesabu muda uliosalia kabla ya kuanza michuano ya Kombe la Dunia mwakani iliyopo jijini Rio de Janeiro imepigwa picha ikiwa imesimama. Ikiwa mpaka sasa imebakia takribani miezi 11 kabla ya kuanza kwa michuano hiyo saa kubwa iliyowekwa na waandaaji katika ufukwe wa Copacabana bado inaonyesha kuwa zimebaki siku 365 kabla ya kuanza kwa tukio hilo kubwa katika soka. Saa hiyo ilionekana kusimama toka alipowasili Papa Francis wiki chache zilizopita na kuvutia mamilioni ya watu aliowahutubia katika ufukwe huo. Katika taarifa yake kamati ya maandalizi ya michuano hiyo ilidai kuwa walikuwa wakijua tatizo la saa hiyo na kuwa kampuni inayohusika na matengenezo inatarajiwa kutatua tatizo hilo mapema. Brazil imekuwa ikikumbwa na changamoto nyingi katika maandalizi ya michuano hiyo hivyo kuibua wasiwasi wa kama miundo mbinu pamoja na viwanja vinavyojengwa kukamilika kwa wakati uliopangwa.

No comments:

Post a Comment