MENEJA mpya wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola amesisitiza kuwa anajali zaidi kuboresha viwango vya wachezaji wake kuliko kushinda mataji. Guardiola mwenye umri wa miaka 42 aliiongoza Barcelona kushinda mataji 14 katika kipindi cha miaka minne ambayo ameinoa klabu hiyo na kuwa kocha aliyepata mafanikio zaidi katika historia. Hatahivyo kocha huyo ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania amesisitiza kuwa kuboresha viwango vya wachezaji mmoja mmoja ni motisha kubwa kwake kuliko kushangilia mataji. Guardiola alionja taji lake la kwanza jana usiku katika michuano ya Kombe la Audi ambapo kikosi chake kilifanikiwa kutoka nyuma na kuifunga Manchester City mwaka mabao 2-1 katika mchezo fainali. Guardiola alichukua nafasi ya Jupp Heynckes kama kocha wa Bayern katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi baada ya kupumzika kwa mwaka mmoja toka alipoondoka Barcelona mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment