Friday, August 2, 2013

SUAREZ ABAKIE LIVERPOOL KWA MSIMU MWINGINE - WRIGHT.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Arsenal, Ian Wright amedai kuwa Luis Suarez anatakiwa kubakia Liverpool na kukataa nafasi ya kuijunga na Arsenal katika usajili wa kipindi hiki cha kiangazi. Liverpool tayari imekataa ofa mbili za Arsenal kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 ambaye anataka kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Akihojiwa Wright amesema atamkaribisha Suarez kwa mikono miwili kama akijunga na Arsenal lakini kama angekuwa yeye angeipa Liverpool msimu mwingine kabla ya kuamua kuondoka. Wright pia alishukuru kuona Arsenal wameamka na kutaka kusajili majina makubwa maana bila ya kufanya hivyo wangekuwa wanaachwa na timu zingine ambazo husajili wachezaji nyota. Suarez ambaye ni raia wa Uruguay tayari ameonyesha nia ya kuondoka Anfield pamoja na kusaini mkataba mpya Agosti mwaka jana.

No comments:

Post a Comment