Monday, September 16, 2013

ALVES ALIJITOLEA KUNIPA INI - ABIDAL.

BEKI wa zamani wa klabu ya Barcelona, Eric Abidal amebainisha kuwa rafiki yake na mchezaji mwenzake wa zamani Dani Alves alijitolewa ini lake kwa ajili ya kupandikizwa kwake. Inajulikana kuwa wawili hao walitengeneza urafiki wa karibu wakati wakicheza wote Camp Nou ambapo ili kuthibitisha ukaribu wao Alves ameacha kutumia namba yake ya kawaida katika fulana yake na kutumia namba 22 iliyokuwa ikitumiwa na Abidal zamani akiwa huko. Abidal amesema urafiki wake na Alves unakwenda mbali zaidi ya kutumia namba ya fulana aliyokuwa akivaa wakati akiwa Barcelona. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliendelea kudai kuwa wakati alipotakiwa kufanyiwa upasuaji Alves alijitolea kumpa ini lake lakini ilishindikana kwasababu alikuwa mchezaji wa kulipwa hivyo ingekuwa ngumu kwake.

No comments:

Post a Comment