Monday, September 16, 2013

CHELSEA HAIWEZI KUPATA MAFANIKIO YA HARAKA - MOURINHO.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameonya kuwa mafanikio katika klabu hiyo hayawezi kuja haraka kufuatia kurejea kwake katika Ligi Kuu kama alivyokua alipotua hapo kwa mara ya kwanza mwaka 2004. Pamoja na kutengeneza nafasi kadhaa, Chelsea walijikuta wakipata kisago cha kufungwa bao 1-0 na Everton Jumamosi na kupelekea kikosi hicho cha Mourinho kupoteza alama tano katika mechi zao nne za kwanza za ligi. Mwaka 2004 wakati akiinoa klabu hiyo kwa mara ya kwanza Mourinho alipoteza alama saba pekee katika mechi 13 za mwanzo za ligi huku akifungwa mechi moja pekee kwa msimu mzima lakini Mreno huyo amesisitiza kuwa mazingira sasa tofauti. Mourinho amesema pamoja na kwamba kikosi kimekuwa tofauti na ilivyokuwa mwaka 2004 lakini hawezi kukubali kuendelea kupata matokeo mabovu.

No comments:

Post a Comment