MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale amepania kupandisha kiwango chake na anaamini kuwa uwepo wa Cristiano Ronaldo, kocha mkuu Carlo Ancelotti na kocha msaidizi Zinedine Zidane utamsadia kwa kiasi kikubwa kufikia lengo lake. Nyota huyo wa kimataifa wa Wales alifunga bao lake la kwanza akiwa na Madrid katika mchezo wa La Liga dhidi ya Villarreal mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo ana uhakika kucheza kwake katika klabu hiyo kutambadilisha na kumpeleka hatua nyingine katika soka lake. Bale amesema Ronaldo ni mchezaji aliyekamilika na atajifunza na kucheza pamoja naye huku akipewa ujuzi kutoka kwa walimu walio bora kama Ancelotti na Zidane. Kwa mara nyingine Bale mwenye miaka 24 amerudia tena kusema kwamba ilikuwa ni ndoto zake kujiunga na Madrid hivyo alipopigiwa siku kueleza kumuhitaji ilikuwa ni siku yenye kubwa kwake na alikuwa akiomba mambo yaende sawa ili afanikiwe kutimiza ndoto zake.
No comments:
Post a Comment