MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti anafikiri kuwa bao alilofunga kiungo mahiri wa klabu hiyo Isco ndilo lililobadilisha matokeo katika ushindi waliopata dhidi ya Galatasaray ya Uturuki. Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Madrid walionekana kubanwa katika dakika za mwanzo lakini walifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 baada ya Isco kufungua karamu hiyo ya mabao katika dakika ya 33. Akihojiwa mara baada ya mechi hiyo Ancelotti alikiri kikosi chake kubanwa katika dakika za mwanzoni lakini bao la Isco liliwatuliza na kuwafanya waweze kumiliki mchezo. Kocha huyo pia aliwapongeza washambuliaji wake Cristiano Ronaldo aliyefunga mabao matatu na Karim Benzema aliyefunga mawili katika mchezo huo kwa kiwango kikubwa walichokionyesha.
No comments:
Post a Comment