Tuesday, September 17, 2013

PLATINI KUTOA UAMUZI WA KUGOMBEA URAIS FIFA MWAKANI.

RAIS wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Michel Platini amebainisha kuwa atatoa uamuzi wake wa kama atagombea nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ifakapo mwakani. Platini aliwaambia wajumbe wa kamati ya utendaji ya UEFA kabla ya mkutano wao huko Dubrovnik, Croatia kwamba hajaamua kitu cha kufanya huko mbele na anahitaji miezi kadhaa ili kufikiria kwa makini. Platini ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Ufaransa aliendelea kudai kuwa atatoa uamuzi wake kabla au baada ya michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Rais wa FIFA Sepp Blatter muda wake unamalizika mwaka 2015 na Platini amekuwa akipewa nafasi ya kuchukua mikoba ya Blatter mwenye umri wa miaka 77 kwa kipindi kirefu.

No comments:

Post a Comment