Thursday, January 9, 2014

ALONSO AKUBALI MKATABA MPYA MADRID.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Real Madrid, Xabi Alonso amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na timu hiyo. Mkataba huyo mpya utamuwezesha Alonso mwenye umri wa miaka 32 kuendelea kubakia Santiago Bernabeu mpaka mwaka 2016. Nyota huyo wa zamani wa Liverpool ambaye mkataba wake ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu alikuwa akihushwa na tetesi za kurejea katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Vyombo vya habari nchini Hispania vimedai kuwa mkataba huo mpya wa nyota utamuwezesha kukunja kitita cha paundi milioni 4.9 kwa msimu huku kukiwa na uwezekano wa kuongezewa mwaka mwingine. Alonso alijiunga na Madrid mwaka 2009 akitokea Liverpool kwa ada ya paundi milioni 30.

No comments:

Post a Comment