Thursday, January 9, 2014

TOURE MBIONI KUNYAKUWA TUZO YA TATU YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA AFRIKA.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure anapewa nafasi kubwa ya kunyakuwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Afrika kwa mara ya tatu mfulizo katika sherehe zinazotarajiwa kufanyika jijini Lagos baadae leo. Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ambaye alinyakuwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Afrika wa BBC Desemba mwaka jana, ameshinda tuzo hizo mara mbili mwaka 2011 na 2012. Didier Drogba anayecheza klabu ya Galatasaray na kiungo wa Chelsea na Nigeria John Obi Mikael ndio wapinzani wake katika tuzo hizo. Pamoja na kutoshinda taji lolote mwaka uliopita, Toure ambaye anatimiza miaka 31 Mei mwaka huu amekuwa akicheza katika kiwango cha juu kwa klabu na timu yake ya taifa.

No comments:

Post a Comment