Tuesday, January 14, 2014

DORTMUND HAINA UWEZO WA KUWABAKISHA NYOTA WAKE - KLOPP.

MENEJA wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp amekiri kuwa klabu hiyo bado itaendelea kuuza wachezaji kutokana na kushindwa kuwazuia wachezaji wake muhimu. Dortmund tayari wameshwapoteza wachezaji kama Shinji Kagawa na Mario Gotze kwa Manchester United na Bayern Munich katika misimu ya hivi karibuni wakati Robert Lewandowski pia akitarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu baada ya kukubalia kusaini mkataba na Bayern. Hata hivyo, Klopp anategemea Dortmund itaendelea na mipangp yake ya maendeleo na kuja kuwa klabu yenye uwezo ya kuwazuia nyota wake kwenda sehemu nyingine katika miaka michache ijayo. Akihojiwa Klopp amesema kwasasa iko wazi kuwa wachezaji wao nyota watakuwa wakiondoka lakini ni jukumu lao kuhakikisha kuwa klabu hiyo inakuwa na kuwavutia wachezaji kuichezea na kupenda kubakia kutoka mishaharamikubwa itakayokuwepo. Klopp ameanza kuinoa Dortmund mwaka 2008 ambapo toka wakati huo ameiongoza timu hiyo kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu nchini Ujerumani, Bundesliga.

No comments:

Post a Comment