NGULI wa soka wa klabu ya Bayern Munich, Stefan Effenberg anaamini kuwa Arsenal inaweza kuwapa wakati mgumu mabingwa hao watetezi kama watatumia aina ya mchezo wa kushambulia katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaochezwa baadae leo. Arsenal watakuwa wenyeji wa Bayern inayonolewa na Pep Guardiola katika Uwanja wa Emirates na kama wakiwafunga Wajerumani hao itakuwa timu ya pili kuifunga Bayern toka Julai 2013. Kulingana na wacheza mahiri kama Mesut Ozil, Olivier Giroud na Santi Carzola waliopo katika kikosi cha Arsene Wenger, Effenberg anaamini kuwa Arsenal inaweza kuwashangaza Bayern katika mchezo huo. Effenberg amesema pamoja na ubora wa Bayern walionao lakini bado wanaudhaifu katika safu yao ya ulinzi na kama Arsenal wakitumia vyema nafasi zao wanaweza kuibuka kidedea katika mchezo huo ingawa bado anawapa nafasi Wajerumani hao.
No comments:
Post a Comment