MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini kuwa Bayern Munich bado haijafikia kiwango cha Barcelona iliyonyakuwa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya chini ya kocha Pep Guardiola. Arsenal watakuwa wenyeji wa mabingwa hao wa Ulaya katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya leo usiku huku wakiwa na kumbukumbu ya kung’olewa katika hatua kama hiyo na Bayern msimu uliopita sambamba na Barcelona ya Guardiola mwaka 2010 na 2011. Ingawa Guardiola amekuwa kocha wa Bayern hivi sasa, Wenger bado anaamini Barcelona ya kipindi kile bado ilikuwa bora kuliko Bayern ambao msimu uliopita walishinda mataji matatu kwa mpigo. Wenger amesema alikuwa akivutiwa zaidi na Barcelona ya kipindi kile kutokana na kasi ya pasi na mchezo wao ni mategemeo yake hawatakutana na hilo watakapocheza na Bayern.
No comments:
Post a Comment