Tuesday, March 11, 2014

BARCELONA NI KLABU YA MAISHA YANGU - FABREGAS.

KIUNGO wa klabu ya Barcelona, Cesc Fabregas amesema klabu hiyo ni ya maisha yake baada ya kuelezea ukaribu aliokuwa nao na wachezaji wenzake. Fabregas alianzia soka lake katika shule ya Barcelona ya La Masia lakini aliondoka na kwenda Arsenal akiwa na umri wa miaka 16 akiwa hajacheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Hata hivyo alirejea na kujiunga na klabu yake hiyo ya utoto mwaka 2011 na baadae kukataa kujiunga na Manchester United majira ya kiangazi mwaka jana na kuendelea kucheza katika timu ambayo amekuwa na mapenzi nayo katika kipindi chate cha maisha yake. Fabregas mwenye umri wa miaka 26 amesema anataka kucheza katika klabu bora duniani ambayo wachezaji wake amekuwa nao toka akiwa mtoto huku wakicheza pamoja pia katika timu ya taifa na haoni nyingine zaidi ya Barcelona. Barcelona inatarajiwa kucheza na Manchester City katika mchezo wa mkondo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho huku wakiwa mbele kwa mabao 2-0 waliyopata katika mechi ya kwanza iliyopigwa Etihad.

No comments:

Post a Comment