Friday, March 14, 2014

JESUS HANA ADABU - SHERWOOD.

MENEJA wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Tim Sherwood amemtuhumu kocha wa Benfica Jorge Jesus kwa kukosa heshima kufuatia kipigo cha mabao 3-1 ilichopata timu yake katika mchezo wa Europa League. Kauli hiyo ya Sherwood imekuja kufuatia Jesus kushangilia bao la tatu la timu yake mbele ya kocha huyo kwa kumnyooshea vidole vitatu akimaanisha idadi ya mabao waliyoshinda. Sherwood alimvaa Jesus kutokana na kitendo hicho na wawili hawakushikana mikono baada ya mchezo huo kumalizika. Kocha huyo amesema anadhani Benfica walicheza vyema na hekima ya hali ya juu lakini ni mbaya kwasababu kocha wao hana hekima hizo. Matokeo hayo yanawafanya Spurs kupata wakati mgumu kusonga mbele katika hatua ya robo fainali na kuongeza siku mbaya kwa kocha huyo baada ya kuandikwa mabao 4-0 na Chelsea katika mchezo wa ligi siku chache zilizopita.

No comments:

Post a Comment