Friday, March 14, 2014

NATAKA KUMALIZIA SOKA LANGU NIKIWA UNITED - VAN PERSIE.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester United, Robin van Persie ameondoa uvumi kuwa anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu huu na kudai kuwa anataka kumalizia soka lake akiwa Old Trafford. Van Persie aliisaidia United kushinda taji la Ligi Kuu katika msimu wake wa kwanza kufuatia uhamisho wake kutoka Arsenal uliogharimu kitita cha paundi milioni 24 lakini amekuwa akicheza chini ya kiwango chini ya kocha mpya David Moyes aliyechukua mikoba ya Sir Alex Ferguson. Hatua ikazusha tetesi kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi anaweza kuuzwa mwishoni mwa msimu wakati Moyes akipanga kusuka upya kikosi chake na Edinson Cavani akiwa mmoja ya wachezaji aliopanga kununua. Lakini Van Persie mwenye umri wa miaka 30 amesema anataka kumalizia miaka yake miwili ya mkataba wake na kuna uwezekano wa kusaini mkataba mwingine kama ilivyokuwa kwa Wayne Rooney. Van Persie amesema ana furaha kuichezea United na angependa kumalizia mkataba wake na hata kusaini mwingine kama itawezekana.

No comments:

Post a Comment