KIUNGO wa klabu ya Valencia, Seydou Keita anaamini kuwa Juventus ni mojawapo ya timu zinazopewa nafasi ya kunyakuwa taji la Europa League lakini anaona bado taji hilo linaweza kuchukuliwa na timu yoyote. Valencia walienguliwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya katika hatua ya makundi lakini walifanikiwa kutinga hatua ya timu 16 bora ya Europa League baada ya kuifunga Trabzonspor. Hata hivyo, Keita anaamini kuwa zipo timu nyingi zinazoweza kuibuka kidedea katika michuano hiyo wakati wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya mabingwa wa Bulgaria Ludogorets baadae leo. Keita amesema pamoja na watu kuipa nafasi Juventus lakini michuano hiyo ni tofauti ligi kwasababu huamuliwa kwa michezo miwili nyumbani na ugenini hivyo anadhani kila ina nafasi ya kushinda.

No comments:
Post a Comment