BONDIA Floyd Mayweather wa Marekani ameendeleza vita vya maneno na Amir Khan wa Uingereza kwa kudai kuwa atapigana na bondia huyo bingwa wa zamani wa dunia kama akifanikiwa kupiga Adrien Broner katika pambano lao. Khan mwenye umri wa miaka 27 alimshambulia Mayweather kwa kuchagua chaguo rahisi wakati alipochagua kupigana na Marcos Maidana badala yake. Mayweather aliwataka mashabiki wake kumchagulia bondia wa kupigana naye kwa kupiga kura na katika kura hizo Khan ndio aliibuka na asilimia kubwa ya kura lakini Mmarekani huyo akaamua kumchagua Maidana aliyepata kura chache. Mayweather aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa twitter kuwa kama Khan akifanikiwa kumchapa Broner katika pambano lao ndipo naye atakapopambana naye.
No comments:
Post a Comment