MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Argentina, Hector Enrique anaamini kuwa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi hataweza kufikia kiwango alichokuwa nacho Diego Maradona enzi zake. Messi mwenye umri wa miaka 26 ambaye anatajwa kama mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya soka akiwa ameshinda tuzo za Ballon d’Or mara nne huku akivunja rekodi za ufungaji katika klabu yake lakini Enrique hadhani kama nyota huyo anaweza kufikia kiwango kama cha Maradona. Enrique amesema Messi hamfikii Maradona hata kidogo, ingawa anampenda na angefurahi kama mwanae angecheza hata kwa asimilia moja kwa uwezo kama wa Messi lakini Maradoka walikuwa mchezaji wa kipekee. Nguli aliendelea kudai kuwa hakutatokea mchezaji kama Maradona tena hata kama Messi akifanikiwa kushinda mataji matatu ya Kombe la Dunia. Enrique alikuwepo katika kikosi cha Argentina kilichonyakuwa taji la michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1986 akiwa sambamba na Maradona.
No comments:
Post a Comment