DEREVA nyota Lewis Hamilton amesema msimu huu mpya wa mashindano ya langalanga ni msimu usiotabirika kuliko yote iliyowahi kutokea. Dereva wa timu ya Marcedes na bingwa wa dunia mwaka 2008 amekuwa akipewa nafasi katika mashindano ya kwanza yatakayofanyika nchini Australia lakini mwenyewe amesema hana uhakika na hilo. Hamilton amesema pamoja na vyombo vya habari kutoa nafasi kubwa kwake na timu yake kufanya vyema msimu huu lakini yeye anadhani ni mapema mno kutabiri kwa kuwa kutakuwa na upinzani mkubwa kutokana na kila timu kujiandaa. Msimu mpya wa mashindano ya langalanga unatarajiwa kuanza mwishoni wa wiki hii huko Australia baada ya kila timu kukamilisha majaribio.

No comments:
Post a Comment