Tuesday, March 18, 2014

NAINGOJA MADRID KWA HAMU - MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amedai kuelekeza nguvu zake kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwa kuifunga Real Madrid wiki ijayo baada ya kuingoza timu hiyo kuidhalilisha Usasuna kwa mabao 7-0 Jumapili iliyopita. Messi aliipiku rekodi ya mabao ya mshambuliaji wa zamani wa Barcelona Paulino Alcantara na kuweka rekodi mpya ya mabao 371 aliyoifungia timu hiyo baada ya kufunga mabao matatu-hat trick katika mchezo huo. Ushindi huo umeifanya Barcelona kutofautiana alama nne na vinara wa La Liga Madrid na Messi anategemea ushindi katika mchezo wa Jumapili utawarudisha katika mbio za ubingwa wa La Liga msimu huu. Messi amesema pamoja na kwamba anategemea mchezo huo kuwa mgumu lakini anaamini wakicheza vyema wanaweza kuibuka na matokeo mazuri.

No comments:

Post a Comment