Tuesday, March 18, 2014

VILLAS-BAS AKUBALI KUINOA ZENIT.

MENEJA wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs na Chelsea, Andre Villas-Boas amekubali mkataba wa miaka miwili kuinoa timu ya Zenit St Petersburg ya Urusi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo Villas-Boas mwenye umri wa miaka 36 ambaye alitimuliwa Spurs Desemba mwaka jana atachukua nafasi ya Luciano Spalletti ambaye ndio kocha wa sasa wa timu hiyo. Taarifa ilitumwa katika mtandao imedai kuwa Zenit imeshafikia makubaliano na kocha huyo ambaye anatarajiwa kutangazwa rasmi Machi 20 mwaka huu. Spalletti ametimuliwa baada ya klabu hiyo kupoteza mchezo wake wa mkondo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa mabao 4-2 nyumbani kwao dhidi ya Borussia Dortmund huku wakiporomoka mpaka nafasi ya pili katika ligi. Sergey Semak aliteuliwa kama kocha wa muda lakini sasa Villas-Boas atakuchukua mikoba hiyo siku moja baada ya mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya Dortmund utakaochezwa kesho.

No comments:

Post a Comment