Tuesday, March 18, 2014

QATAR YAKANUSHA KUTOA HONGO.

KAMATI ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar imekanusha taarifa kuwa ilitoa hongo kwa ajili ya kupata nafasi ya kuandaa michuano hiyo mwaka 2022. Hatua hiyo imekuja kufuatia gezeti la Daily Telegraph la Uingereza kudai kuwa makamu wa rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Jack Warner na familia yake walilipwa zaidi ya paundi milioni moja na kampuni inayomilikiwa na ofisa wa zamani wa soka kutoka Qatar. Gazeti hilo lilidai kuwa Warner na watoto wake wa kiume walionekana kulipwa kiasi cha paundi milioni 1.2 na kampuni inayomilikiwa na Mohamed Bin Hammam. Bin Hammam alikuwa ni mmoja ya wajumbe wenye nguvu FIFA kwa miaka mingi lakini alifungiwa maisha kujishughulisha na mambo ya michezo na shirikisho hilo kufuatia tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi wakati wakiwa rais wa Shirikisho la Soka barani Asia. Katika taarifa yake kamati hiyo imesema Qatar ilifuata taratibu zilizowekwa na FIFA katika kufanya maombi ya kutaka nafasi hiyo kwa mujibu wa sheria zilizowekwa hivyo hawahusiki na tuhuma hizo zlizotolewa na gazeti hilo.

No comments:

Post a Comment