NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard amemtaka mmiliki wa klabu hiyo kumpatia mkataba mpya Brendan Rodgers haraka kabla ili kuzuia kuchukuliwa na vilabu vingine vikubwa. Rodgers ameigeuza Liverpool kutoka nafasi ya saba bora ilipokuwa imezoeleka mpaka kuwa bingwa wa kutegemewa ndani ya miezi 12 huku akikiongoza kikosi hicho kuidhalilisha Manchester United katika Uwanja wao wa Old Trafford kwa kuifunga mabao 3-0 Jumapili. Lakini Rodgers ambaye ni raia wa Ireland ya Kaskazini anatarajiwa kuingia mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake wa sasa mwishoni mwa msimu huu na tayari kumeshakuwa na tetesi za kuwindwa na Barcelona kuchukua nafasi ya Gerardo Martino ambaye yuko kikaangoni. Gerrard amesema anafurahia kocha huyo kuwepo hapo na anategemea kuwa tayari juhudi zinafanyika kuhakikisha anasaini mkataba mpya haraka ili aendelee kuifundisha timu hiyo.

No comments:
Post a Comment