Friday, March 14, 2014

STURRIDGE AIKWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI.

MSHAMBULIAJI nyota wa Liverpool, Daniel Sturridge ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa mwezi wa Ligi Kuu nchini Uingereza kwa mara ya pili msimu huu. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 ambaye pia alishinda tuzo hiyo Agosti mwaka jana alipewa tuzo hiyo kwa kufunga mabao matano na kutoa pasi mbili za mwisho katika mechi za Liverpool mwezi uliopita. Sam Allardyce mwenye umri wa miaka 59 naye alipata tuzo ya kocha bora wa mwezi baada ya kuisaidia West Ham United kupata alama 12 mwezi Februari. West Ham ilipata ushindi katika mechi zake nne mfululizo dhidi ya Swansea City, Aston Villa, Norwich City na Southampton na kukwea mpaka nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment