MCHEZAJI nyota wa tenisi anayeshika namba mbili katika orodha za ubora duniani, Novak Djokovic amefanikiwa kunyakuwa taji lake la tatu katika michuano ya wazi ya Italia baada ya kumgaragaza Rafael Nadal. Djokovic mwenye umri wa miaka 26 raia wa Serbia alifanikiwa kumtandika Nadal bingwa mtetezi wa michuano hiyo kwa alama 4-6 6-3 6-3 kwa muda wa saa mbili na dakika 19. Ushindi huo unamfanya Djokovic kumtambia Nadala raia wa Hispania kwa mechi ya tatu mfululizo walizokutakana hivi karibuni. Michuano hiyo imekuwa kama kupasha misuli kwa wachezaji hao kwa ajili ya mashindano makubwa ya wazi ya Ufaransa ambayo inatarajiwa kuanza Jumapili inayokuja.
No comments:
Post a Comment