DEREVA nyota wa mashindano ya langalanga kutoka Uingereza Lewis Hamilton amesema sasa atakuwa akishambulia katika kinyang’anyiro cha ubingwa na dereva mwenzake Nico Rosberg baada ya kuibuka kidedea katika mashindano ya British Grand Prix. Ushindi huo umemfanya Hamilton kupunguza pengo la alama kati yake na dereva mwenzake huyo wa Marcedes kutoka alama 29 mpaka nne baada ya Rosberg kulazimika kujitoa kwa mara ya kwanza msimu huu. Hamilton amesema msukumo uko juu lakini anafikiri kuwa sasa ni wakati muafaka wa kuanza mapambano kwa ajili ya ubingwa wa dunia. Hamilton alishinda mbio hizo zilizofanyika katika ardhi yao pamoja na kuanza katika nafasi ya sita kufuatia kufanya makosa katika mashindano ya kufuzu yaliyomfanya kujitoa katika mzunguko wa mwisho.
No comments:
Post a Comment