KLABU ya Hull City imefanikiwa kunyakuwa winga mahiti Tom Ince mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni mtoto wa nahodha wa zamani wa Uingereza Paul Ince kutoka klabu ya Blackpool. Klabu hiyo ilitangaza usajili wa nyota huyo katka mtandao wake na kuongeza kuwa wamempa mkataba wa miaka miwili. Taarifa hiyo haikuweka wazi ada waliyokubaliana katika mauzo ya mchezaji huo. Hull ambao walifungwa na Arsenal katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA Mei mwaka huu, wanafundishwa na meneja Steve Bruce ambaye alicheza na Paul Ince katika timu ya Manchester United kati ya mwaka 1989 mpaka 1995.
No comments:
Post a Comment