KLABU ya Galatasaray imethibitisha kuwa Cesare Prandelli ndiye kocha mpya wa timu hiyo ikiwa ni wiki mbili baada ya kujiuzulu wadhifa wake kama kocha wa timu ya taifa ya Italia kwa kushindwa kufanya vyema katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil. Klabu hiyo kongwe ya Uturuki imebainisha taarifa hizo kupitia katika mtandao wake leo na kueleza kuwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 56 atachukua nafasi ya Roberto Mancini kwa kipindi cha miaka miwili ijayo. Prandelli anatarajiwa kuwasili jijini Instabul baadae leo kwa ajili ya kusaini mkataba huo na kutembelea kambi ya mazoezi ya timu hiyo kabla ya kukutana na wachezaji hapo kesho. Mancini ambaye alitimuliwa mara baada ya kumalizika kwa msimu uliopita aliiwezesha klabu hiyo kushika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo.
No comments:
Post a Comment