KLABU ya Paris Saint-Germain-PSG inajipanga kutoa fungu kwa ajili ya kumsajili golikipa wa Chelsea, Petr Cech. Kipa huyo mkongwe amekuwa na upinzani mkali wa kugombea namba katika kikosi cha Chelsea baada ya kusugua benchi na nafasi yake kuchukuliwa na Thibaut Courtois katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Burnley Jumatatu. Hatua hiyo inaweza kumshawishi Cech kutafuta klabu mpya katika kipindi hiki cha mwisho wa usajili wa kiangazi baada ya kuwa kipa namba moja wa Chelsea kwa miaka 10. Klabu za Real Madrid na Monaco ni mojawapo ya vilabu vinavyofuatilia kwa karibu nyendo za nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 huku PSG wakitarajiwa kuwa wa kwanza kutoa ofa kwa ajili ya kumsajili. Meneja wa Chelsea Jose Mourinho pamoja na kumpa nafasi Courtois lakini amedai kuwa bado anataka kumpakisha mkogwe huyo katika kikosi chake.
No comments:
Post a Comment