Wednesday, August 20, 2014

NFF YATANGAZA KIKOSI CHA SUPER EAGLES BILA KOCHA.

SHIRIKISHO la Soka la Nigeria-NFF limetangaza kuwa hakuna kocha yoyote wa muda atayeteuliwa kwa ajili ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles kuelekea mchezo wao wa kufuzu Mataifa ya Afrika dhidi ya Congo Brazzaville. Mashabiki wengi wa soka wan chi hiyo wamehoji jana wakati NFF ilipotoa orodha ya wachezaji 23 kuiwakilisha nchi hiyo kwa ajili ya mchezo wao huo utakaochezwa Septemba 6 mwaka huu huku wakiwa bado hawajatangaza jina la kocha mpya. Ilikuwa inahisiwa kuwa NFF watalazimika kumtaja kocha wa muda kwa ajili ya Super Eagles wakati mazungumzo ya mkataba mpya na Keshi ikiaminika kukwama. Rais wa NFF, Alhaji Aminu Maigari amesema kwasasa hawafikiri ktafuta kocha wa muda kwasababu bado wako katika mazungumzo na Keshi na orodha waliyotaja kwa ajili ya mchezo na Congo imetumwa kwao na Keshi. Keshi alichukua mikoba ya kuinoa Super Eagles mwaka 2011 na kuingoza kufanikiwa kunyakuwa taji la Mataifa ya Afrika mwaka jana nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment