Tuesday, January 6, 2015

AFCON 2015: TUNISIA KUMKOSA BEN-HATIRA.

SHIRIKISHO la Soka la Tunisia limetangaza kuwa kiungo wa klabu ya hertha Berlin, Anis Ben-Hatira ataikosa michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon kutokana na kuwa majeruhi. Mapema benchi la ufundi la timu ya taifa ya nchi hiyo lilitangaza kuwa ushiriki wa kiungo huyo uko katika hatihati. Baada ya kufanyiwa vipimo vya afya jana shirikisho hilo lilijiridhisha kuwa Ben-Hatira hatakuwepo katika kikosi cha nchi hiyo kitakachokwenda Guinea ya Ikweta baadae mwezi huu. Shirikisho hilo limetangaza kuwa kiungo wa ushambuliaji wa klabu ya Africain Tijan Belaid ndiye atakayeziba bafasi ya Ben-Hatira. Tunisia wamepangwa katika kundi moja sambamba na timu za Zambia, Cape Verde na DR Congo katika michuano hiyo ya Afcon.

No comments:

Post a Comment