Friday, January 16, 2015

BAADA YA KUING'OA REAL MADRID KOMBE LA MFALME, SIMEONE ATAMBA TORRES KIDUME.

MENEJA wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone amesema Fernando Torres amerejea katika timu akiwa kidume baada ya mshambuliaji huyo kufunga mabao mawili jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 30 aliondoka Atletico na kwenda Liverpool mwaka 2007. Torres alisajiliwa tena na Atletico mapema mwezi huu na kufunga mabao mawili katika mchezo waliotoka sre ya mabao 2-2 dhidi ya Real Madrid na kuwang’oa mabingwa hao watetezi wa Kombe la Mfalme kwa jumla ya mabao 4-2. Simeone amesema Torres aliondoka akiwa amepevuka lakini sasa amekuwa mwanaume kamili hivyo anafurahi kuwa naye katika kikosi chake. Torres amefunga mabao 84 katika mechi 214 za La Liga alizoichezea Atletico kuanzia mwaka 2001 hadi 2007 kabla ya kwenda Liverpool, Chelsea na baadae AC Milan.

No comments:

Post a Comment