KLABU ya Manchester City imemuongeza mkataba kiungo Frank Lampard ambao utamalizika mwishoni mwa msimu huu. Mkataba wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36 kutoka klabu ya New York City ulimalizika jana lakini sasa ataendelea kuwemo mpaka majira ya kiangazi na kumfanya kukosa mwanzo wa msimu wa Ligi Kuu nchini Marekani-MLS. Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza amefunga mabao sita katika mechi 17 alizoichezea City msimu huu. Lampard alisajiliwa na New York baada ya kuachwa na Chelsea Juni mwaka huu ambapo muda wake rasmi wa kuanza kucheza soka utathibitishwa baadae kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment