MENEJA wa klabu ya Manchester United amethibitisha kuwa Rafael na Luke Shaw wote wamepata majeruhi katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Yeovil Town. Wachezaji wote hao wawili walitolewa nje katika kipindi cha mapumziko katika mchezo huo wa mzunguko wa tatu uliofanyika katika Uwanja wa Huish Park na nafasi zao kuchukuliwa na Jonny Evans na Juan Mata. Hatua hiyo ilipelekea United kubadili mfumo wao kutoka kutumia mabeki watano na kubakisha wannne lakini mabadailiko hayo hayakuleta madhara kwani timu hiyo iliibuka na ushindi mnono wa mabao 2-0. Van Gaal amebainisha kuwa pamoja na majeruhi waliyopata wachezaji wake hao lakini amefurahishwa na kiwango cha timu yake katika mchezo huo wa ugenini. Kocha huyo amesema siku zote ni vigumu kucheza na timu za daraja la chini kwani zinakuwa zimepania mchezo lakini anashukuru kwa ushindi waliopata kwani umeaongezea hali yakujiamini katika mechi zao ugenini.

No comments:
Post a Comment