NAHODHA wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard amedai kuwa angeweza kukubali kubakia katika timu hiyo kama angepewa ofa ya mkataba mpya mapema. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 alitangaza wiki iliyopita kuondoka Anfield mwishoni mwa msimu huu na kuhamia katika Ligi Kuu ya Soka nchini Marekani-MLS. Mwishoni mwa wiki iliyopita Gerrard alidai kuwa uamuzi wake wa kuondoka ulikuja wakati meneja wa klabu hiyo Brendan Rodgers alipomhabalisha kuwa hatakuwa akimpanga katika kila mchezo. Hata hivyo, Gerrard amesema kuwa kama angewekewa ofa ya mkataba mpya wakati wakijiandaa na msimu huu hana kwamba angesaini kwani aliamua kustaafu soka la kimataifa ili kuhamishia nguvu zake Liverpool. Nyota huyo amesema pamoja na hayo hana haja ya kumnyooshea kidole yeyote na uamuzi wake aliochukua haukutokana na hasira kwani ameona wakati wake wa kuondoka hapo ulikuwa umefika.

No comments:
Post a Comment