Tuesday, January 6, 2015

GOLIKIPA WA ARSENAL ATANDIKWA FAINI YA PAUNDI 20,000 KWA KOSA LA KUVUTA SIGARA.

GOLIKIPA wa kikosi cha kwanza cha klabu ya Arsenal, Wolciech Szczesny ametozwa faini ya paundi 20,000. Adhabu hiyo imemuangukia baada ya kukutwa na kosa la kuvuta sigara muda mchache baada ya kupoteza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Southampton. Kitendo hicho cha uvutaji sigara kilimkasirisha meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger na kuamua kumuangushia adhabu hiyo. Kiungo Jack Wilshere pamoja na nahodha wa zamani wa klabu hiyo William Gallas waliwahi kukumbwa na tatizo kama hilo la uvutaji wa sigara.

No comments:

Post a Comment